Beyond Coffee

Karibu Lunji

Lunji Coffee Estate ni shamba la kahawa lililopo katika mkoa wa Mbeya, Tanzania.  Kimo cha zaidi ya meta 1500, rutuba na hali ya hewa inayofaa, kwa miaka mingi vimewezesha kilimo cha mojawapo ya  kahawa bora katika bara la Afrika. Kahawa ya Lunji ilijipatia tuzo la "Coffee of the year" mwaka 2013 London, nchini Uingereza pamoja na tuzo mbali mbali miaka ya nyuma.

 

Shamba lipo karibu na milima ya  Mbeya Mountain Range, chini ya mlima Mbeya Peak  wenye kimo cha meta 2839. Mwonekano wa mlima huo mkubwa na pori la Mbeya Mountain Range, pamoja na wingi wa mimea na wanyama mbali mbali, vimepabariki Lunji na mandhari yenye uzuri wa kustaajabisha.