Beyond Coffee

Kahawa ya Lunji

Ugunduzi na usambazaji wa kinywanji cha kawa katika nchi za uarabuni na ulaya si siri tena. Hapa Lunji vivyo hivyo tunafanya ugunduzi mkubwa wa historia ya kahawa yetu na  jinsi gani je ilipata kufika katika eneo hili la Tanzania. Mawasiliano na wazee wa zamani pamoja na familia zao yanawezesha kupeleleza historia ya shamba na kahawa iliyopo.

Mwisho wa karne ya 19, wamisionari waliingiza miche ya kahawa Afrika Mashariki kutoka kwenye kisiwa cha Bourbon ( Leo kinaitwa La Reunion). Aina hii ya kahawa inayokwenda kwa jina la Bourbon ilipandwa kwanza Morogoro na kutoka hapo ilisambazwa katika mikoa mingine Tanzania. Wamisionari wa shirika la kimoravian ( Herrnhuter Mission ) walileta miche ya kwanza Mbeya na kuipanda kwenye mashamba ya misheni Utengule. Utengule ni kitongoji karibu na Lunji, umbali wa kilometa 5 kutoka Lunji

Mashamba ya kwanza Lunji yalipandwa kwa kutumia aina hii ya Bourbon.

Hali ya hewa inayofaa imewezesha kilimo cha kahawa yenye ubora wa hali ya juu aina ya Arabika

Katika miaka iliyopita miti iliyopandwa zamani imechanganywa, na sehemu zingine imebadirishwa na aina mbali mbali za kahawa.  Huu mchanganyiko wa aina  mbali mbali umeipatia kahawa ya Lunji utamu wa kipekee na wenye wingi na uzito wa ladha. 

 Msimu wa Kuvuna

Aina za Kahawa 

Utengenezaji wetu

Mei-Septemba

Bourbon (SL28, N39, French Mission)

 Kuchuma kwa mkono


Typica (SL34, Blue Mountain) 

 Kukoboa na kuosha


Catimor&Rume Sudan Hybrids

 Kukausha juani


Wasiliana nasi kama kuna maswali yeyote kuhusu kahawa, tupo tayari kujibu kadri ya uwezo wetu.