Beyond Coffee

Masaa 3.5 kupanda, masaa 3.0 kushuka

Kwa wale wapendao zoezi la kupanda milima, bila shaka mlima Mbeya Peak ni changamoto nzuri na pia mahali pazuri pakuburudika na mimea na pori la kupendeza. Njia iendayo kiileleni hupita kwenye msitu wa hifadhi ya Mbeya Forest Reserve. Hapa huweza kuona mimea ya kipekee isiyopatikana tena kwa wingi sehemu nyingine.

Baada ya kufika kileleni, kuna mandhari nzuri  ya Lunji Estate , jiji la Mbeya, Mbalizi, Songwe, Milima ya Uporoto, Chunya,  ziwa Magadi, na kwenye siku nzuri hata ziwa Rukwa huonekana. Ziwa Rukwa husifika kwa wingi wa mamba majini mwake.

Msimu mzuri wa kupanda:

15.Mei-15.Novemba

Kuna uwezekano wa mvua katika miezi mingine


Wasiliana nasi kabla ya safari, na sisi tupo tayari kuandaa guide mwaminifu kwaajili ya kuongoza njia


Utaratibu:

-Magari yanaweza kuegeshwa bure  shambani 

(Lunji Estate haitowajibika kwa uharibifu wa vyombo)

-Malipo ya guide yanapaswa kukubaliana na yeye mwenyewe 

-KWA SABABU YA USALAMA TAFADHALI TUJULISHE KUJA KWAKO NA PIA KUONDOKA KWAKO