Beyond Coffee

Tuliko toka

Kama kila mmoja hata  Lunji pia ina historia, na historia yake ni ya kipekee na ya kuvutia.

1898, wakati Tanzania ilikuwa chini ya ukoloni wa wajerumani, maarufu kama  "Deutsch Ost-Afrika" ,  Bwana  Emil Koestlin mhamiaji wa kutoka Ujerumani allinunua kiwanja ambapo leo panaitwa Lunji. Licha ya kuwepo kwa wananchi wachache wa kabila la kisafwa, hili eneo lilikuwa ni pori kubwa.  Emil Koestlin aliliita shamba lake  "Mbeya-Hof" na alijishughulisha na kilimo cha  hekta 3 za kahawa, ufugaji wa punda na alikuwa ana n´gombe wafikao 1500. Pia alifanya ufugaji wa nguruwe kadhaa, kilimo cha mahindi, shayiri,  na aina mbali mbali ya miti ya matunda.


Baada ya Ujerumani kupigwa na kushindwa vita ya kwanza ya dunia na Tanzania kukabidhiwa kwa waingereza, Bwana Koestlin alilazimika kuliacha shamba lake na aliwekwa mbaroni nchini Misri kabla ya kukimbilia Marekani Kusini. Hatimaye alijaribu kurudi Afrika lakini aliishia kuuwawa Msumbiji baada ya kuingilia kati mgogoro wa kikabila nchini humo.

Mwisho wa vita ulileta mabadiriko mengi kwa Tanzania na mabadiriko mengi kwa Mbeya-hof. 

Waingereza waliyofwata waligundua mapema uwezo wa kuzalisha kahawa mahali hapa. Ardhi yenye rutuba na hali ya hewa inayofaa viliruhusu kuendeleza ulimaji wa kahawa.

Mwaka 1928 waingereza walisafisha pori ili kupanua mashamba ya kahawa. Kuanzia hapo eneo hili lilibatizwa jina la  Lunji Estate. Inawezekana kwamba neno  "Lunji" lina uasili wake katika neno la kisafwa la  "Ilunji" kwaajili ya aina ya mti unaopatikana hapa.


 Lunji leo...

Leo Lunji ni shamba lenye ukubwa wa wastani, wafanya kazi wafikao 30, na vibarua 150 wakati wa msimu wa kuvuna.  Shamba linaendeshwa na kusimamiwa na Clemens na Stella Maier kwa zaidi ya miaka 20 sasa, na hufanya kazi yake kisheria kama mali ya Clemens Maier na Thomas Plattner toka mwaka 1994.  Pamoja na Kahawa pia Lunji inajisifia kilimo cha maparachichi, apples,  ufugaji wa kuku wa mayai, nguruwe na ukuzi wa miti aina mbali mbali ya matunda.


General data:

 Ukubwa (Kahawa)

92 ha

Kimo       

1500-1700 m

Kiasi cha mvua kwa mwaka

 1150 ml

Halijoto     

Mchana 23C°  /  Usiku 13C°

Topografia

Milimani, chini ya Mlima Mbeya peak (2839m

Ardhi

rutuba nzuri, mchanganyiko wa udongo mchanga na mabaki ya viumbehai,  asidi kwa mbali, ph 4.7-5.7